KESI YA KUBAKA.. NELLY AACHIWA HURU

Imeripotiwa kuwa kesi ya Ubakaji iliyokuwa ikimkabili rapa Nelly, imefutwa na Waendesha Mashtaka.

Sababu kuu iliyotajwa ni kukosa ushirikiano wa Mshtaki ambaye alikaririwa kujitoa kwenye kesi hiyo.

Mnamo October 8 mwaka huu, #Nelly alitiwa nguvuni mara baada ya Mwanamke mmoja kudai kubakwa na rapa huyo walipokuwa kwenye Bus la ziara jijini Washington.

Hata hivyo Mwanasheria wa Nelly, bwana Scott Rosenblum aliibuka na kukanusha taarifa hizo akidai zimesukwa kumchafua mteja wake.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.