Mwalimu atuhumiwa kubaka wanafunzi 9

Jeshi la Polisi wilayani Tarime mkoani Mara limemkamata na kumfikisha mahakamani mwalimu wa shule ya msingi Itiryo iliyopo Kata ya Ingwe,Samweli Mariba Daniel (29) kwa tuhuma za kuwabaka watoto 9 wa darasa la kwanza.


Kamishna Msaidizi wa polisi, Henry Mwaibambe amesema kuwa walishirikiana na halmashauri ya Tarime na tulifanikiwa kumkamata huyo mwalimu akijiandaa kutoroka kwenda nje ya nchi.
‘Vitendo hivyo vimefanyika katio ya tarehe 30 hadi tarehe 6 baada ya taarifa kufika kwenye vyombo vya dola mwalimu huyu alikamatwa katika mazingira magumu sana, juhudi kubwa kabisa za jeshi la polisi zilifanyika na kwakushirikiana na halmashauri ya wilaya ya Tarime na tulifanikiwa kumkamata huyo mwalimu akijiandaa kutoroka kwenda nje ya nchi,’ alisema Kamanda Mwaibambe.]

‘Amefikishwa mahakamani jinai 682 upepelezi wa shauri hili umekamilika na kila ushahidi umekamilika tumemfikisha mahahakamani katiki ya watoto hawa 9 watatu aliwadhalilisha kingono.’

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.