Picha: Staa wa Korea Kusini aliyejinyonga azikwa jana

Hatimaye msanii wa muziki kutoka kundi la Shinee Korea Kusini, Kim Jong-hyun ambaye alijinyonga Jumatatu hii amezikwa leo.

Mwili wa marehemu Jonghyun ambaye alikuwa na umri wa miaka 27 ulikuwa umehifadhiwa katika hospitali ya Asan Medical Center kabla ya kuzikwa leo mjini Seoul.
Watu mbalimbali wamehudhuria katika mazishi hayo wakiwemo wasanii wenzake wa kundi la Shinee na dada yake ambaye alitumiwa ujumbe wa simu na marehemu usiku kabla ya tukio.

Dada wa marehemu Kim Jong-hyun akiwa ameshika picha ya kaka yake huku akilia kwa uchunguBaadhi ya watu waliohudhuria mazishi ya Kim Jong-hyun wakilia kwa uchungu


Wasanii wengine wa kundi la Shinee wakiwa wamebeba jeneza la marehemu Kim Jong-hyun

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.