Rayvanny, Derulo, Montana kutikisa duniaNa: Omary Ramsey

Staa wa Bongo Fleva, Rayvanny, ameahidi kufanya vizuri kwenye anga la kimataifa baada ya msanii nyota wa Marekani, Jason Derulo, kumshirikisha kwenye toleo mbadala (remix) ya wimbo wake wa Tip Toe, Imeelezwa.

Wimbo huo ambao awali, Jason Derulo, aliutoa mwanzoni mwa mwezi huu na mpaka sasa hivi video yake imetazamwa na watu milioni 10, umerudiwa tena huko Los Angeles, Marekani na ndani yake atasikika Rayvanny, Jason Derulo, mwenyewe pamoja na staa wa singo ya Unforgettable, French Montana.

“Watu wangu kaeni tayari kwa Tip Toe Remix, Mungu ni mwema,” alisema Rayvanny, akiwapa taarifa mashabiki zake juu ya ujio wa ngoma hiyo.

Awali, Jason Derulo, alimshukuru Rayvanny kwa kushiriki kwenye wimbo huo akisema: "Asante kaka kwa kutia baraka kwenye wimbo wangu". Rayvanny naye alimjibu kwa kusema: "Kweli kaka ngoja tuionyeshe dunia kitu wanachotakiwa kupata".

Wawili hao kwa mara ya kwanza walikutana kwenye msimu uliopita wa Coke Studio na tayari wamefanya wimbo huo unaotarajia kutoka hivi karibuni.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.