Sasa Unaweza Kuagiza Albamu #MoneyMondays Ya Vanessa Mdee

Wiki hii imekua poa zaidi kwa wadau wa muziki Bongo hasa mashabiki wa Cash Madame Vanessa Mdee ambae anajipanga kuiachia Albamu yake hiyo ambayo imekua ikisubiriwa kwa muda mrefu.
Vanessa ambae amekua akiiongelea Albamu hiyo kwa miaka kadhaa sasa ameamua kuweka hadharani Artwork, tarehe ya kutoka na List ya nyimbo 18 tutakazozisikia zikiwa zimeshirikisha wasanii wengine wakali ambao ni Joh Makini, Mr P (Peter wa Psquare), Tahpha, Cassper Nyovest, Gnako, Radio & Weasal, Maua Sama, Tommy Flavour, Mohombi, Konshens, Reekadobanks, K.O na JUX.

Kwa watumiaji wa App ya BoomPlay wanaweza kuweka Oda mapema kabla ya January 15 ambayo ni siku inayotarajiwa kuanza kupatikana rasmi.
Mbali na Money Mondays kingine ambacho Vee Money ametangaza wiki hii ni deal ya mkwanja mrefu aliyosaini na Universal Music Group.

(Credit Mp3tz)

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.