TIMAYA HUYOO KWENYE GRAMMY!

Muimbaji wa Nigeria Timaya ametajwa kwenye kipengele cha Tuzo za Grammy 2018.

Staa huyo wa miondoko ya dancehall ametajwa kwenye kipengele cha Best Reggae Album, hii ni baada ya ushiriki wake kwenye album ya kundi la Morgan Heritage iitwayo 'Avrekedabra' ambayo imetajwa kuwania kipengele hicho.

Kama Morgan Heritage wakishinda basi watamuwezesha Timaya kuwa M-Nigeria wa kwanza kuchukua Tuzo hiyo yenye heshima kubwa duniani.

Hii si mara ya kwanza kwa Wanaigeria kutajwa kwenye Tuzo hizo, mwaka 2016 WizKid na Kah-Lo waliwania lakini walitoka patupu.


(Credit InfoHD) 

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.