Alikiba na Diamond ni biashara za watu – Dully Sykes

Msanii mkongwe wa Bongo Flava, Dully Sykes amesema hataki kuingilia ‘ugomvi’ wa Diamond na Alikiba kwa sababu wao ni biashara ya watu.Muimbaji huyo anayefanya vizuri na ngoma Bombardier amesema Diamond na Alikiba ni kama klab za Simba na Yanga kusema zisiwepo zije timu nyingine ni kuua biashara.

“Sisi Tanzania Diamond na Alikiba ni biashara za watu na sitaki kuingilia kwa sababu utakuwa unaingilia kitu ambacho ni biashara unaweza kusema leo Simba na Yanga zisiwepo nani atakubali wakati watu ndio wanafanyia biashara,” amesema
.
“Nafikiri siwezi kuingilia ugomvi wa Diamond na Alikiba, sitaki hata kuingilia ugomvi wao, Alikiba ni mdogo wangu nampenda, Diamond ni mdogo wangu nampenda, kwa upande wangu sioni tofauti zao,” amesisitiza.

Ameongeza tangu alipotaka kuwapatanisha kupitia wimbo na ikashindakana amekuwa akijiweka kando na mvutano wao.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.