Gari mpya ya Sanchez ndani ya Man United ni hatari

Ukitaja jina la Alexis Sanchez utakuwa unazungumzia benki inayotembe. Hilo ni kutokana na fedha atakazokuwa anapokea kama mshahara wake kwa wiki kwenye klabu yake mpya ya Manchester United.Katika kuonyesha thamani yake hiyo kama mchezaji anayelipwa fedha nyingi katika ligi ya Uingereza, Sanchez ameamua kumiliki gari la kifahari zaidi na lenye thamani kubwa.Gari hilo ni Bentley GT yenye thamani ya paundi 150,000 ambapo ni zaidi ya shilingi milioni 475 za kitanzania.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.