Iggy Azalea atangaza kolabo na Quavo

Iggy Azalea amekuwa na wakati mgumu katika kuachia albamu yake ya Digital Distortion, albamu hiyo ilitakiwa kutolewa tarehe 30 Juni mwaka jana lakini ilipigwa chini na Def Jam Records.Msanii huyo alidai kwamba Mkurugenzi Mkuu wa Def Jam Steve Bartels amekataa kuachia ngoma zake na tukio hilo lilitokea baada ya ngoma yake ‘Switch’ aliyomshirikisha mbrazil aitwaye Anitta kushindwa kufanya vizuri.Iggy sasa ameamua kuanza upya katika mwaka huu kwa kutangaza kuachia ngoma iitwayo ‘Switch’.Raia huyo wa Australia ametangaza leo kwamba ngoma hiyo atamshirikisha msanii Quavo kutoka kwenye kikundi cha Migos. Msanii huyo ametangaza kuwa tarehe 1 Februari mwaka huu ndio siku atakayo iachia ngoma hiyo, Iggy pia amethibitisha kufanya kolabo hiyo na Quavo kwa kumjibu shabiki wake katika mtandao wa Twitter.No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.