Mshambuliaji tegemezi wa Liverpool atangaza kuhama

Ikiwa ni wiki chache zimepita tangu klabu ya Liverpool kuondokewa na mshambuliaji wao Philippe Coutinho sasa pengo lingine huenda likawapata tena baada ya mchezaji wao mwingine, Daniel Sturridge kutangaza kuwa anataka kuondoka klabuni hapo.

Tokeo la picha la daniel sturridge, Liverpool team
Daniel Sturridge
Imeelezwa kuwa Sturridge anataka kuelekea Hispania kwa mkopo kunako klabu ya Sevilla ambapo Liverpool wanataka wamuuze kwa moja kwa moja kwa Euro milioni 30.

Kwa mujibu wa gazeti la Marca la Uhispania limeandika kuwa klabu ya Sevilla ipo tayari kumlipa Sturridge mshahara wake wote kwa msimu huu.

Sturridge amekuwa akiugulia majeraha tangu Desemba 6, 2017 alipoumia wakati Liverpool ilipoiadhibu klabu ya Spartak Moscow goli 7-0 kwenye mchezo wa Klabu Bingwa barani Ulaya.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.