Thierry Henry na Sanchez wawakana hadharani mashabiki wa Arsenal

Ikiwa asilimia kubwa ya mashabiki wa Arsenal wanaamini kuwa mshambuliaji wao wa zamani Thierry Henry ndiye aliyemshawishi aliyekuwa mshambuliaji wao, Alexis Sanchez kuhamia Manchester United, hatimaye wawili hao wamekanusha taarifa hizo.


Alexis Sanchez na Thierry Henry
Thierry Henry ndiye aliyekuwa wa kwanza kukanusha uvumi huo unaonezwa na mashabiki wa Arsenal ambapo kupitia ukurasa wake wa Twitter alitweet kwa kusema “Ninajua sihitaji kuelezea hili kwa mashabiki wengi wa Arsenal lakini kinyume na uvumi hakuna muda wowote 

nilimwambia Alexis Sanchez aondoke Arsenal. Sikujua kwamba angeenda kusajiliwa na Man Utd mpaka nilipoona kwenye habari kama wengine.

Baadaye naye Sanchez kupitia ukurasa wake wa Twitter alikazia ishu hiyo kwa kuandika “Nataka kufafanua kwamba Henry hakuniambia kamwe kuondoka kwenye klabu hiyo (Arsenal), bali yalikuwa ni maamuzi yangu binafsi, Anaipenda klabu na siku moja itakuwa vizuri nikimuona kama kocha wa arsenal kwa sababu anaipenda klabu“.

Sanchez amejiunga na klabu ya Manchester United kwa kubadilishana na Henrikh Mkhitaryan kutokea Manchester United kwenda Arsenal.

No comments

Theme images by lobaaaato. Powered by Blogger.